7 Aprili 2025 - 23:13
Source: Parstoday
Shirika la kutetea haki za binadamu la US lazilaumu nchi za Magharibi kwa 'kufanya mauaji ya kimbari' huko Gaza

Kundi la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu nchini Marekani limeikosoa Marekani, Israel, Canada na nchi nyingine za Magharibi kwa kuhusika na "mauaji ya kimbari" ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Taarifa iliyochapishwa jana Jumapili kwenye mtandao wa kijamii wa X na Taasisi ya Lemkin ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari, ililaani "uungaji mkono wa Magharibi kwa mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya wanaume, wanawake na watoto wa Kipalestina wasio na hatia huko Gaza "ni makosa ya kimaadili ambayo yanapaswa kuzitesa nchi hizi milele." 

"Uzuiaji wa mauaji ya kimbari umekufa huko Gaza," imesema taarifa ya The Lemkin Institute for Genocide Prevention, na kuongeza kuwa, "Mauaji ya kimbari sasa ndio utaratibu uliopo duniani."

Taasisi hiyo ya kutetea haki za binadamu yenye makao yake nchini Marekani imeonya kuwa watu walio madarakani wanataka kuweka umma katika giza kuhusiana na mauaji ya kimbari yanayoendelea licha ya viongozi wa Israel wenyewe kukiri mara kwa mara kwamba wanalenga kuwaua Wapalestina wote.

Imesisitiza kuwa ni wakati muafaka kwa jamii ya dunia kusimama na kuchukua hatua dhidi ya wale wanaotekeleza mauaji ya kimbari ya Israel yanayoongozwa na Marekani dhidi ya Wapalestina.

Mnamo Oktoba 2023, Taasisi ya Lemkin ilianza kuonya kwamba vikosi vya jeshi la utawala wa Israel vimeanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha